MH. DKT RAIS JAKAYA KIKWETE AMALIZA ZIARA BRAZIL

KIKWETE AWAAGA WABRAZIL BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE
RAIS MRISHO JAKAYA KIKWETE AKIWAAGA WABRAZIL
RAIS Jakaya Kikwete anahitimisha ziara yake leo nchini Brazil kwa kufungua mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hiyo na Tanzania, wenye lengo la kuhamasisha uwekezaji nchini.Katika ziara hiyo, Rais Jakaya amepata nafasi ya kuitangaza Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo hatua zilizopigwa kwa masuala ya ubia na uwazi.

Pia, alitembelea sehemu mbalimbali ikiwa ni miongoni mwa harakati za kuchochea uwekezaji kuja nchini.
Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana ilisema, baadhi ya hatua ambazo Serikali imepiga katika ubia wa uwazi, ni shughuli za Bunge la kuendeshwa kwa uwazi na kutangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari.

“Watanzania wanapata fursa ya kuona wawakilishi wao wakijadili na kuuliza maswali kutoka serikalini, bajeti za Serikali zinapitiwa na kujadiliwa na Kamati za Bunge na Bunge kwa ujumla, uhuru mkubwa wa vyombo vya habari na kuwekwa wazi kwa shughuli za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambako ripoti hutolewa na kujadiliwa kwa uwazi bungeni,” alisema Rais. 

Pia, alisema sheria za uhuru wa kupata habari, vyombo vya habari tayari vimeanza kuziangalia upya za kutangaza mali kwa maofisa wa Serikali.

Rais Kikwete aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa Serikali yake ni waumini wakubwa wa ushirikishaji watu kwa masuala nyeti yanayohusu nchi yao, ndiyo sababu mwaka jana alianzisha jitihada za mchakato wa katiba.

Mpango wa ubia wa uwazi serikalini, unalengo la kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki zaidi kuamua mambo yanayowahusu, kupitia vyama visivyo vya kiserikali na jamii.

Ubia huu unashirikisha kwa usawa wawakilishi wa Serikali kwa upande mmoja na wawakilishi wa asasi zisizo za Serikali kwa upande mwingine.Nchi 55 duniani zimejiunga na mpango huo hadi kufikia sasa kutoka nane mwaka jana ulipoanza. 

Leave a Reply