Mzungu wa Azam FC ataka kumkalia juu simba

Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall.



PAMOJA na kwamba hapo awali alikuwa akitangaza kuwa kikosi chake kinahitaji nafasi ya pili tu, Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amegeuka na kusema sasa vita yao ni dhidi ya Simba.


Hall, raia wa Uingereza, amesema watafanya kila linalowezekana kuchuana na Simba hadi hatua ya mwisho, ili waone kama watatwaa ubingwa au watashika nafasi ya pili.
“Ukiangalia tuna nafasi ya kutwaa ubingwa, tunatakiwa kushinda mechi zote tatu. Itategemea pia Simba itacheza vipi karata zake, tukishindwa basi angalau nafasi ya pili,” alisema Hall.
“Kila mchezaji anajua tuko katika nafasi gani, ubingwa au nafasi ya pili vyote vinawezekana na haitakuwa kazi rahisi.”
Hall alisema yupo kwenye maandalizi ya mechi yao dhidi Mtibwa Sugar, itakayochezwa kesho, ambayo inaweza kuwa na majibu sahihi.
Azam ipo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 50.

Leave a Reply