Mawaziri wanaotakiwa kujiuzuru kutokana ubadhilifu wa mali ya UMMA


Kujiuzuru kwa mawaziri hao ni matokeo ya hoja ya mheshimiwa mbunge Zitto Kabwe ambae katika kikao kilichopita aliliomba bunge kupiga kura ya kutokuwana imani na waziri mkuu kwa kushindwa kuwadhibiti mawaziri wake na kuruhusu uzembe, ubadhirifu na ufisadi ndani ya serikali. Kat...ika maelezo yake mheshimiwa Zitto Kabwe aliwaomba wabunge kuweka itikadi za vyama vyao pembeni ili kuinusuru nchi na baada ya kikao cha bunge akaendesha kampeni ya kukusanyasaini za wabunge ili kutimiza masharti ya kanuni za bunge yanayotakiwa kufuatwa ili kuweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.. YALIYOTOKEA J.mosi Mheshimiwa Naibu Spika, bila kumwajibisha Waziri Mkuu hawa Mawaziri waliotajwa hawatatoka na wasipotoka madudu haya yatarudia. Kwa hiyo Mbunge yoyote mwenye uchungu na ubadhirifu, Mbunge yoyote ambaye anakereka na watoto kwenye Jimbo lake kukaa chini, Mbunge yoyote anayekereka na madawa kuharibiwa na MSD na MSD kushindwa kupeleka madawa kwenye vijiji vyetu, nampa taarifa kwamba kuanzia kesho tunakusanya sahihi za Wabunge 70,ili siku ya Jumatatu tutoe hoja hapa Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. ( Makofi ) Mheshimiwa Naibu Spika, na kipindi hiki tunakitoa Mawaziri wote ambao wapo implicated kwenye taarifa hizi waweze kuona ama wao, au wamtoe rehani Waziri Mkuu. ( Makofi ) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wabunge wote wenye uchungu kuanzia kesho tutakuwa pale mlangoni, sahihi zinazohitajika ni 70 tu, kwa ajili ya kuleta hapa Bungeni na Wabunge wanahitajika kupitisha hilo azimio ni nusu tu ya Wabunge, 50 plus one .Tukifanya hivyo tutakuwa tumewapa heshima wananchi wetu, wataona kweli tumewatendea haki badala ya kupiga kelele bila ya kuchukua action. ( Makofi ) Mawaziri saba waachia ngazi... Mhe. George Mkuchika Mawaziri saba wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania wameandika barua za kujiuzuru nafasi zao kufuatia tuhuma nzito za ubadhirifu wa mali ya umma zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya mawaziri hao. KIKAO CHA DHARURA BAADA YA BUNGE Kujiuzuru kwa mawaziri hao kumefuatia kikao cha dharula kilichoitishwa na waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha bunge mjini Dodoma. Mhe. Mizengo Pinda Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda yupo katika hatari ya kupoteza nafasi yake baada ya wabunge 75 kutia saini za kupendekeza kupigwa kura ya kutokuwa na imani nae. Majina ya mawaziri waliojiuzulu usiku wa jumamosi yametajwa hapo juu na picha zao kama zinavyoonekana.

One Response so far.

  1. Anonymous says:

    Hi! I juѕt wanted to аsk if you ever hаve
    аny problems with hаckers? My lаst blog (ωordpress) was hаckеԁ and I ended uρ losing a few months of hard wоrk ԁue to no
    ԁаtа bаckuρ. Do you have аnу methoԁs to prеvent hackerѕ?


    my wеbpage forex trading
    My web page: Forex Tip

Leave a Reply